Wananchi wa Kata ya Bolisa Halmashauri ya Kondoa Mjini wametakakiwa kujitokeza bila kuogopa ili waweze kupata huduma ya msaada wa kisheria ua Mama Samia kwani huduma hii inatolewa bure kwa makundi yote bila ubaguzi
Akizungumza wakati wa zoezi la utoaji wa Elimu kata kwa kata, Msajili Msaidizi na Mratibu wa Huduma hiyo kwa Halmashauri ya Kondoa TC, Glory Kavishe amesema Huduma hii inawafikia wananchi wote bila ubaguzi kwa Kata zote 8 na Mitaa yote 36 zilizopo katika Halmashauri hiyo
“Huduma ya Kampeni ya Samia Legal Aid Campaign imewafikia kwa Awamu ya pili na inawafikia Wananchi wote bila Ubaguzi kwa Kata zote 8 na Mitaa 36” Amesema Kavishe
Aidha, Kavishe ameshukuru kwa Huduma hii ya Msaada wa Kisheria kwani Wananchi wengi wanamatatizo, migogoro wanaogopa kuiwasilisha sehemu husika hivyo kwa kufika Maeneo hayo na kuwapatia Elimu wameweza kufunguka na kuelezea Matatizo yanayo wakabili
“Tunashukuru Kwa hii huduma, tunawafikia Wananchi kwasababu Wananchi wengi wanamatatizo, Wananchi wengi wana migogoro wanaogopa lakini kwa kufika huku wanajitahidi kufunguka na kuwaeleza Migogoro yao” amesema Kavishe.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma hizo, akiwemo Diwani wa Kata hiyo Ramla Abedi pamoja na Mohamedi Hamza wameeleza kufurahishwa na kampeni hiyo kwani huko zamani kupata Huduma za Kisheria ulipaswa kulipia lakini kwa sasa kupitia huduma hii wanahudumiwa bure bila gharama zozote zile.
Katika kampeni hiyo itakayo tekelezwa kwa muda wa siku 15 katika Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma, wananchi wanapatiwa elimu na msaada wa kisheria wa utatuzi wa migogoro mbalimbali ikiwemo ndoa, ardhi, mirathi, matunzo ya watoto, migogoro ya mipaka pamoja na masuala ya ukatili wa kijinsia na kingono.


0 Comments