Ticker

6/recent/ticker-posts

MAMLAKA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI YASHIRIKI KIKAMILIFU WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, ameelekeza wakuu wa taasisi za umma kutenga fedha na kuhakikisha huduma mbalimbali zinapatikana katika mabanda yao wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ili wananchi wanufaike moja kwa moja na huduma zinazotolewa.

Prof. Shemdoe ametoa maelekezo hayo Juni 23, 2026 wakati akifunga Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Amesema maonesho hayo yanapaswa kuwa jukwaa la kutoa huduma, elimu na ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi badala ya kuwa sehemu ya maonesho pekee.

Miongoni mwa taasisi zilizoshiriki katika maonesho hayo ni Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, pamoja na taasisi nyingine za umma zilizotumia fursa hiyo kutoa huduma na elimu kwa wananchi.

Maonesho hayo yamefanyika sambamba na maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma Afrika, ambayo hutambua mchango wa watumishi wa umma katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.










Post a Comment

0 Comments