Ticker

6/recent/ticker-posts

WAKIMBIZI WAMUOMBA RAIS SAMIA NA WATANZANIA KULINDA AMANI YA NCHINI



Jumla ya Wakimbizi 155,811 wanaohifadhiwa katika maeneo mbalimbali nchini wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote kulinda amani iliyopo nchini huku wakiweka wazi madhara ya kutoweka kwa amani ambapo wamejikuta wakipoteza kila kitu na kukimbilia nchini Tanzania.


Wametoa kaulihiyo  jijini Dar es Salaam wakati wakizungumza  katika Maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo mwezi Juni,kila mwaka huku kauli mbiu ya mwaka huu ikisema “Hadi Kila Mtu awe Salama”




Waziri Katambi akizungumza mbele ya Wakimbizi wanaoishi jijini Dar es Salaam ambao waliwawakilisha jumla ya wakimbizi 155,811  wanaoishi katika maeneo mbalimbali nchini amesema nchi ya Tanzania ijifunze kwa yaliyotokea nchi jirani huku akitoa ahadi ya serikali ya kuwahudumia Wakimbizi mahali popote walipo na kusisitiza Serikali ya Tanzania itahakikisha amani iliyopo inaendelea kuwepo ili kuweza kuwapa fursa wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji na uchumi.

Post a Comment

0 Comments