Ticker

6/recent/ticker-posts

JUKWAA LA USHIRIKA DODOMA LAGUSA ELIMU YA JUU

Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoa wa Dodoma   limezinduliwa rasmi leo Mei 29, 2026 kwa kutoa Hundi ya kiasi cha Shillingi Milioni 14,690,200 kwa Wanafunzi 29 wa Vyuo vikuu vya Dodoma ikiwemo UDOM, Mipango na Hombolo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, leo Mei 29,2026 Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Dodoma, Joseph Chitinka, amesema jukwaa hilo ni sehemu ya kuimarisha mshikamano na kuhakikisha ushirika unachangia kuboresha maisha ya wananchi, hususani wanafunzi kutoka familia zenye mazingira magumu.

Vyama vya Ushirika mkoa wa Dodoma limezindua rasmi Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Dodoma likilenga kuimarisha utekelezaji wa misingi ya ushirika, hususani msingi wa saba unaohusu kusaidia jamii na makundi yenye uhitaji.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo la Ushirika  Ibrahim  Sumbe, amesema hatua hiyo ni katika kuimarisha uhusiano wa Vyama vya Ushirika na  kurudisha faida ya utendaji  Jamii pamoja.

Maadhisho ya Jukwaa hilo yataendelea kwa ratiba nyingine ikiwemo Bonanza la Michezo pamoja na Mkutano wa majadiliano ya masuala ya Ushirika tarehe 5-6 Juni, 2026 Jijini Dodoma.







Post a Comment

0 Comments