Ticker

6/recent/ticker-posts

KIOHONGOSI : WAPUUZIENI WANASIASA WANAOWASHAWISHI KUWACHUKIA POLISI



Na Mwandishi wetu,Mara

Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi amewataka Watanzania kuwapuuza wanasiasa wanaowashawishi kuwachukia askari wa Jeshi la Polisi, akieleza kuwa askari hao wana jukumu muhimu la kulinda usalama wa raia na mali zao.


Kihongosi ametoa kauli hiyo jana Mei 16, 2026 alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Nyamwaga, katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini mkoani Mara, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne katika mkoa huo.


Amesema jamii inapaswa kuthamini mchango wa vyombo vya ulinzi na usalama badala ya kushawishiwa kuvichukia, akisisitiza kuwa amani na utulivu ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa.


“Bila amani hakuna maendeleo. Wananchi wanapaswa kushirikiana na vyombo vya dola kuhakikisha usalama wa maeneo yao unaimarika muda wote,” amesema Kihongosi.


Aidha, amewataka wakazi wa Tarime kujiepusha na wanasiasa wanaochochea vurugu na migogoro, akieleza kuwa kauli za uchochezi zinaweza kuhatarisha mshikamano wa jamii pamoja na maendeleo ya wananchi.

Post a Comment

0 Comments