Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHİ MLOWA WANUFAIKA NA KAMPENİ YA MSAADA WA KİSHERİA YA MAMASAMIA

Wananchi wa eneo la Mlowa, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, wamejitokeza kupata huduma za msaada wa kisheria zinazotolewa bure kupitia Kampeni ya Samia Legal Aid inayoendelea mkoani humo.

Timu ya watoa huduma wa kisheria imetembelea Mlowa Bwawani na Mlowa Bwawani ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa awamu ya pili ya kampeni hiyo, ambayo ilianza Mei 1, 2026 na inatarajiwa kukamilika Mei 15 mwaka huu.

Katika siku ya leo Mei 2 2026, wananchi wamepatiwa elimu ya kisheria pamoja na ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala mbalimbali yanayowakabili katika maisha yao ya kila siku. Miongoni mwa masuala yaliyopewa uzito ni pamoja na migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi, matunzo ya watoto, pamoja na migogoro ya mipaka.

Aidha, timu hiyo imeendelea kutoa msaada katika kushughulikia changamoto zinazohusiana na ukatili wa kijinsia na kingono, huku ikihamasisha jamii kuchukua hatua stahiki dhidi ya vitendo hivyo.

Wananchi waliopata huduma hizo wameeleza kuwa kampeni hiyo imekuja wakati muafaka, ikiwasaidia kupata mwanga wa kisheria na mbinu za kutatua migogoro yao kwa njia sahihi.









Post a Comment

0 Comments