Wananchi wa Chinugulu Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wameendelea kunufaika na huduma za msaada wa kisheria zinazotolewa bure kupitia Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama, huku wengi wakijitokeza kupata ushauri, elimu na ufumbuzi wa changamoto zao.
Awamu ya pili ya kampeni hiyo imeanza rasmi Mei 1, 2026, na inatarajiwa kuendelea hadi Mei 15 katika Mkoa wa Dodoma. Timu ya wataalamu mbalimbali imeanza shughuli zake katika eneo la Chinugulu, ambapo imekuwa ikitoa elimu kwa umma pamoja na kushughulikia migogoro mbalimbali.
Wananchi waliojitokeza wameipongeza serikali kwa kuendeleza kampeni hiyo, wakisema imekuwa msaada mkubwa kwao kwani wengi wao hawakuwa na uwezo wa kumudu gharama za huduma za kisheria.
Kampeni ya Samia Legal Aid inalenga kuongeza uelewa wa kisheria kwa wananchi na kuhakikisha wanapata haki zao kwa urahisi, hivyo kuchangia kupunguza migogoro katika jamii.










0 Comments