Ticker

6/recent/ticker-posts

UTEKELEZAJI AWAMU YA PILI SAMIA LEGAL AID UMEAMZA RASMI DODOMA


Katika kuhakikisha wananchi wote wanapata haki kwa wakati na Usawa, Wizara ya Katiba na Sheria imeanza kutekeleza rasmi Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Awamu ya Pili Mkoani Dodoma kwa lengo la kutoa huduma za Msaada wa kisheria kwa wanachi wote hasa wale wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za Huduma za kisheria. 

Katika awamu hii ya pili ya utekelezaji  Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi mbalimbali katika mnyororo wa haki jinai zinazoshiriki kutekeleza Kampeni hii zitatoa huduma mbalimbali ikiwemo ushauri wa kisheria, utatuzi wa migogoro mbalimbali ikiwemo Migogoro ya Ardhi, ndoa, mirathi, matunzo ya watoto na Changamoto zinazohusiana na ukatili wa kijinsia. 

Elimu ya Sheria na Uraia pia itatolewa kwa wananchi na huduma zote zitatolewa Bure.

Post a Comment

0 Comments