Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AMTUNUKU IGP WAMBURA ASILIMIA 70 KWA MAGEUZI YA KINIDHAMU KWA JESHI LA POLISI


Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amemtunuku alama ya asilimia 70 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura. Rais ametoa alama hizo kama pongezi kwa jinsi jeshi hilo lilivyofanyia kazi maelekezo yake kikamilifu, hasa katika kusimamia nidhamu, ukakamavu na mwonekano wa askari nchini kote.


Akizungumza kwenye hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi la Polisi, kozi namba 1 ya mwaka 2025/2026, Kurasini Jijini Dar es Salaam, akieleza kufurahishwa kwake na mabadiliko makubwa ya kimwili na kiutendaji yaliyooneshwa na askari waliohitimu. 


"Nimeona Wambura kwamba maelekezo niliyokupa umeyafanyia kazi. Nimeona miili ya askari wetu jinsi ilivyo minyoofu, hakuna mwenye kitambi cha mbele wala nyuma. Vijana wote wamenyooka vizuri na wanapendeza. Sasa mimi nikikupa maksi hapo nakupa asilimia 70." Amesema Rais Samia.


Pamoja na pongezi hizo kubwa, Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia amelitaka Jeshi la Polisi Nchini kutobweteka na mafanikio hayo ya sasa, bali kuongeza juhudi ili kumalizia changamoto zilizobaki. Rais alifafanua kuwa bado kuna asilimia 30 ya maboresho inayotakiwa kufanyiwa kazi ili kufikia ufanisi wa asilimia 100.

Post a Comment

0 Comments