Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam
Waziri wa mambo ya ndani Nchini Tanzania Mhe. Patrobas Katambi ameahidi kuwa Wizara hiyo na Vyombo vya ulinzi vitaendelea kuwa na utii usiogawanyika kwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza nidhamu pia kwa vyombo vya ulinzi na usalama na kuchukua hatua kali kwa wale watakaoenda kinyume na taratibu na sheria za Tanzania.
"Ahadi yetu kwako Mhe. Rais, tutahakikisha tunakuwa na utii kwako usiogawanyika katika kutekeleza majukumu yote ambayo umetupatia katika Wizara hii. Vyombo vya ulinzi na usama navyo vitaendelea kufanya kazi zake kwa nidhamu na kuhakikisha wale wanaoenda kinyume na nidhamu tunachukua hatua na mara zote tutatenda kwa haki bila upendeleo, tutafanya kwa mujibu wa sheria na taratibu kama jinsi ambavyo umekuwa ukituelekeza Mhe. Rais juu ya namna ya kutenda ili watanzania waweze kupata haki na wafurahie kuwa katika taifa lao na usalama." Amesema Waziri Katambi.
Amezungumzia pia weledi kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na maboresho ya maslahi ya Askari polisi pamoja na upandishwaji madaraja kwa Askari hao, akisema Mataifa na dunia kwasasa inajifunza kutoka Tanzania.

0 Comments