Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI KATAMBI AAHIDI HATUA ZA KISHERIA KWA ASKARI WANAOKIUKA TARATIBU NA SHERIA



Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya ndani Nchini Tanzania Mhe. Patrobas Katambi mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi Mei 28, 2026 amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua kwa Askari Polisi wanaokiuka misingi na utii wa kazi zao ili kuendelea kulinda taswira njema ya Jeshi la Polisi dhidi ya wachache wanaochafua taswira hiyo.


Waziri Katambi ameyasema hayo kwenye hafla iliyoongozwa na Rais Samia ya kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi la Polisi, kozi namba 1 ya mwaka 2025/2026, Kurasini Jijini Dar es Salaam, akisema anatambua pia hatua mbalimbali ambazo zimeendelea kuchukuliwa kwa Askari Polisi wasiofuata taratibu na kutii viapo vyao.


"Natambua zipo hatua mbalimbali zimechukuliwa dhidi ya askari ambao walienda kinyume na taratibu lakini tushukuru kwamba wengi wanafuata misingi na viapo vyao katika utendaji wa kazi. Mhe. Rais hili tukuahidi, tutaendelea kusimamia lakini pia iwe ahadi ya utii kwa askari kwako kwamba tumapoenda kufanya kazi hizi kwa mujibu wa sheria tukaendelee kuishi katika viapo vyetu. Tumeapa kwa Mwenyenzi Mungu, tumeapa kwa Katiba yetu na tumeapa kwenye Mamlaka ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." Amesema Waziri Katambi.

Post a Comment

0 Comments