Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AAGIZA UIMARISHAJI WA POLISI JAMII ILI KULINDA AMANI NA USALAMA WA NCHI



Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kulingana na Katiba ya Tanzania kifungu cha 265(1) ulinzi na usalama wa nchi ni jukumu la kila Mtanzania, suala ambalo lilichagiza kuanzisha Polisi jamii kama nguzo muhimu katika utekelezaji wa takwa hilo la Kikatiba.


Rais Dkt. Samia ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 28, 2026 kwenye hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi la Polisi, kozi namba 1 ya mwaka 2025/2026, Kurasini Jijini Dar es Salaam, akimpongeza pia Kamishna wa Polisi Jamii kwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu kwa ushirikiano na Wananchi wa Tanzania, akimtaka kusimamia vyema eneo lake la kiungozi.


"Kifungu cha 265(1) cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinasema ulinzi na usalama wa Nchi ni jukumu la kila Mtanzania. Uanzishwaji wa Polisi jamii ni miongoni mwa nguzo muhimu katika muelekeo huo, nami nimpongeze kamishna aliyeteuliwa kushikilia eneo hilo na nimtake asimamie vizuri eneo hili kwasababu usalama wetu na ulinzi wetu utatokana na wananchi wenyewe na taarifa zitakazotokana na wananchi wenyewe na hata wananchi mkiwafundisha vizuri watalindana wenyewe na hata kutoa taarifa za kiuhalifu pale zinapotokea." Amesema Rais Samia.

Post a Comment

0 Comments