Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKOSA MAKUBWA YA JINAI YAMEPUNGUA NCHINI- KATAMBI


Na Mwandishi wetu,Dodoma

Waziri wa Mambo ya ndani Nchini Tanzania Mhe. Patrobas Katambi, ameliambia Bunge la Tanzania kuwa katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili 2026, makosa makubwa ya jinai 39,027 yalitolewa taarifa katika Vituo mbalimbali vya Polisi ikilinganishwa na makosa 40,022 yaliyotolewa taarifa katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2024/25.

"Kupungua kwa makosa hayo kumetokana na kuongezeka kwa uelewa na ushirikiano wa Jamji katika kubaini na kuzuia uhalifu." Amesema Waziri Katambi wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya mambo ya ndani kwa mwaka 2026/27 leo Mei 25, 2026 Bungeni, Dodoma.

Kuelekea mwaka 2026/27, Waziri Katambi amesema Wizara yake kupitia Jeshi la Polisi litaendelea kudhibiti uhalifu Nchini, ikiwemo matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na udukuzi wa taarifa za kimtandao kwa kukamilisha uanzishwaji wa Ofisi za Kanda za upelelezi wa makosa ya uhalifu wa Kimtandao katika Jiji la Dodoma na Zanzibar.

Ameeleza pia kuhuys mpango wa kuimarisha kikosi Maalumu cha kudhibiti taarifa potofu na uchochezi mtandaoni pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu athari za kusambaza taarifa za uongo.

Post a Comment

0 Comments